Australorp wanastahimili mazingira tofauti, kama
kuku wa kienyeji aliye zoeleka nchini Tanzania. Na ni wazuri kwa ufugaji
huria, kwa kuwaachia nje wajitafutie chakula wenyewe. Ingawa
wanajulikana kwa sifa yao ya utagaji mayai mengi, lakini kuku hawa
wanafaa kwa nyama pia, kwani huwa na nyama nyingi sana (dual purpose
chickens)
Kuku hawa huweza kumpatia mfugaji faida kubwa, kwani
ni wazuri kwa biashara ya mayai na nyama pia. Hawana sifa nzuri ya
kulalia mayai, lakini akilalia hutotoa vifaranga vingi, na ni wazuri kwa
uleaji wa vifaranga hivyo.
Utagaji wao wa mayai unakaribia ule
wa kuku wa kizungu. Kuku hawa ni wakubwa, wazito, na wanamvuto sana
kuwaangalia. Wanapendeza pia kwa ufugaji mdogo, katika mazingira ya
nyumbani. Wana michirizi ya kijani pale wanapomulikwa kwenye mwanga
mkali wa jua.
Kwa wastani Black Australorp, hufikisha mayai 250
kwa mwaka, wakiwa katika mazimgira mazuri. Kuku hawa ni wapole na rafiki
kwa binadamu. Black Australorp ni wagumu, hawapati magonjwa mara kwa
mara, hivyo basi huvumilia magonjwa ya aina nyingi, na hawachagui
chakula. Wanakula vyakula wanavyo kula kuku wengine wa kienyeji. Huanza
kutaga wakiwa na umri wa miezi mitano na nusu hadi sita.
Jogoo hufikisha kilo 3.5 – 5.0 na
Temba/hen hufikisha kilo 3.0 – 3.7
Ushauri. Kama ndio unaanza ufugaji wa kuku, chagua Black Australorp. Hakika, utanufaika.
nahitaji hawa kuku nawezaje kuwapata?jogoo 6
ReplyDeleteVifaranga wanapatikana kwa shiringi ngap?
ReplyDeleteNice..
ReplyDeleteVifaranga wacheki jamaa wanaitwa uriocross and pure breeding wapo arusha wanauza vifaranga 3000https://www.instagram.com/p/BQvWxa0FKq1/
ReplyDeleteHow will I get chickens of malawi in dar?
ReplyDeleteNawapataje hawa nahitaji kama 300
Delete